Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi kutoka kaunti ya kisii wanaiomba serikali ya kaunti hiyo kuzipa majina barabara zote ambazo hukarabatiwa na serikali ya kaunti majina ya viongozi wa eneo hilo kama njia moja ya kuwakumbuka.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatatu katika eneo la Sombogo, bunge la Kitutu Chache, wakaazi hao wakiongozwa na Jairus Ondieki walipendekeza kuwa kama njia moja ya kuwakumbuka viongonzi wa eneo la Kisii katika siku za usoni, sharti barabara hizo zipewe majina kama vile barabara ya James Ongwae.

“Katika miji mingine mikuu unapata barabara zimepatiwa majina kama Kenyatta Avenue, na miji mingine mbona sisi wakisii tusifanye hivyo?”auliza Benard Ongeri mkaazi.

“Tunaomba barabara zote katika kaunti ya Kisii, haswa zile hukarabatiwa na serikali ya kaunti kupatiwa majina kama James Ongwae Road, hiyo itawezesha kizazi kijacho kubaini viongonzi kama magavana ambao wameongoza kaunti mbalimbali nchini,” alihoji Justus Nchogu, mkaazi mwingine.

Aidha, wakaazi hao wameomba ombi hilo kutiliwa maanani ili lianze kufanya kazi rasmi katika kaunti ya Kisii, na kuongeza kuwa gavana wa kaunti hiyo amefanya maendeleo zaidi kuliko baadhi ya kaunti zingine huku wakisema miradi mbalimba imeinuliwa na gavana kama ile ya maji, masomo na barabara.

Kwa sasa ni jukumu la serikali ya kaunti hiyo kuona na kutathmini ombi hilo kupitishwa kuanza kufanya kazi.