Wakaazi wa eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini, Kaunti ya Kisii wametishia kuandamana kutokana na ukosefu wa uwazi kwa ugawaji wa basari kutoka hazina ya ustawi maeneo bunge katika bunge hilo.
Wakiongea na mwandishi huy siku ya Jumanne katika uwanja wa shule ya upili ya wasichana ya Marani, wadi ya Marani, wakaazi hao, ambao watoto wao wako katika vyuo mbalimbali nchini, walikiri kuwa hawajawahi pokea hizo pesa za basari kwa wakati mrefu, ilihali wanajaza fomu za basari kila kuchao.
“Mimi ni mjane na sijawai pokezwa hizo pesa za basari kwa mtoto wangu anayesomea tahaluma ya ualimu mwaka wa pili katika chuo cha Moi Eldoret,” alihoji Frolence Simba, mzazi.
Baadhi ya wakaazi wa eneo bunge hilo walisema katika ugawaji wa pesa hizo za hazina ya CDF, wanafunzi hukabidhiwa pesa hizo killingana na jinsi wanatambulikana, jambo ambalo limewapelekea wakaazi wa eneo hilo kumwomba mbunge wao Jimmy Angwenyi kuingilia kati .
Wakati huo huo, wakaazi hao wameomba ofisi ya CDF ya eneo bunge hilo kuonyesha uwazi wanapogawa pesa hizo za basari, na wazipeane kwa wakati ufaaao.
Aidha, walisema wamepeana mda wa juma moja ili swala hilo kushughulikiwa kikamilifu, la sivyo watachukua mkondo mwingine wa kuandamana.