Wakaazi Wadi ya Nyota katika eneo bunge la Kuresoi Kaskazini wamelalama kupuuzwa na Mbunge wa eneo hilo Moses Cheboi, wakisema hawajanufaika na miradi ya CDF pamoja na hazina ya Uwezo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wenyeji wa eneo la Langwenda wameuliza kusitishwa kwa mradi ya kujenga mitaro ya maji, katika barabara moja ambayo inaunganisha wakaazi hao na maeneo mengine wakisema serikali ya kaunti ilikuwa imetuma wanakandarasi ili kuweka daraja badala ya mitaro hiyo.

Wakaazi hao wamesema hawataki mitaro hiyo iekezwe kwa ufadhili wa pesa za CDF, wakisema ni heri barabara hiyo kuwekwa daraja kama ilivyopendekezwa na mwakilishi wa eneo hilo, Njuguna Gichamu ili kurahisisha usafiri.

Aidha wananchi hao wamewashutumu wasimamizi wa CDF kwa kile walichotaja kama kuingilia miradi inayotekelezwa na serikali ya kaunti wakisema maafisa hao wamezua mzozo wa kimaendeleo baada ya kuvuruga mradi huo uliokuwa utekelezwe na serikali ya jimbo.

Gichamu kwa upande wake amesema shilingi nusu milioni zilizowekezwa na CDF katika mradi huo, hazitakamilisha kazi hiyo akisema serikali ya jimbo iliwekea mradi wa kujenga daraja kwa kima cha shilling millioni 1.3.

Kiongozi huyo amemtaka mbunge wa eneo hilo kutekeleza majukumu yake kikamilifu badala ya kuingilia miradi ambayo tayari inatekelezwa na serikali ya kaunti ya Nakuru.