Wakaazi wa Wadi ya Magogoni, katika eneo bunge la Kisauni, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuchimbiwa shimo la kupitisha maji taka.
Wakaazi hao kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakilalamikia kuwepo kwa maji machafu ya mvua yanayofurika kutoka kwa mabomba mengine na kupitia karibu na makaazi yao.
Akiongea katika wadi hiyo alipokuwa akikagua shimo hilo, Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba alisema kuwa alichukua hatua hiyo kama njia mja ya kuipa afya ya wakaazi hao kipao mbele.
Alisema kuwa wakaazi wamekuwa wakishuhudia mafuriko kila kunaponyesha, hali aliyosema kuwa huenda ikahatarisha afya yao.
"Shimo hili la kupitisha maji machafu litasaidia wakaazi kujinga dhidi ya maradhi ambayo huenda yakasababishwa na maji machafu,” alisema Bedzimba.
Wakaazi wa Kisauni walimshukuru mbunge wao kwa kuwajali na kuwaepusha dhidi ya maradhi mbalimbali kama vile kipindupindu.