Wakaazi wa mtaa wa Manyani viungani mwa mji wa Nakuru wanatishia kuandamana kulalamikia hali mbovu ya mitaro ya kuputisha maji taka.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wanadai kwamba mitaro iliyoundwa eneo hilo haiwezi patisha maji hayo kwani inalemewa na nguvu ya maji hasua kunaponyesha.

"Hii mitaro imekuwa kero kila wakati kuna mvua, maji yanailemea na kutapakaa barabarani," alisema John Kamau, mmoja wa wakaazi.

Naye Jane Nyanchama anayefanya biashara ya mboga na matunda kwenye mtaa huo alisema kuwa mvua inaponyesha inakuwa kero hata kwa biashara yake.

"Mvua ikinyesha mitaro inapasuka kwanza hapa Manyani na ikifanya hivyo maji yanajaa katika hiki kibanda changu.

"Walitoa wito kwa mwakilishi wadi hiyo Vitalis Okello kushughulikia swala hilo la sivyo wataandamana.

Kwa mujibu wao, iwapo swala hili halitashughulikiwa itakuwa kero hata zaidi na athari kwa watoto kwani maji hayo yanaweza kusababisha maafa.