Wakaazi wa Wadi ya Marani eneo Bunge la Kitutu Chache Kaskazini Kaunti ya Kisii wameshukuru Serikali ya Kaunti hiyo kupitia Mwakilishi wao Dennis Ombachi kwa kulikarabati barabara ya kutoka Marani Junction kuelekea Kiareni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Barabara hiyo imekuwa kero kwa wakaazi wa eneo hilo kwa muda mrefu haswa mvua inaponyesha, mradi ambayo imewafurahisha sana.

Wakiongea na Mwandishi wa Habari huyu siku ya Jumanne asubuhi, baadhi ya wakaazi kutoka Lokesheni ya Mwagichana walisema kuwa barabara hiyo imekuwa mbovu kwa muda mrefu na ni baadhi ya barabara za kufanya shughuli za uchukuzi kwa hali ya juu kwani linatumiwa na wanabiashara kuelekea soko la Nyakoe.

“Tunashukuru Mwakilishi Ombachi kwa kulikarabati barabara hili na tunamwomba akarabati barabara zingine katika eneo hili ili shughuli za uchukuzi ziwe rahisi kwetu,” alihoji Geoffrey Nyandika, mmoja wa wakaazi wa eneo hilo.

Ikumbukwe kuwa ni siku nne tu baada ya Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae kusema Serikali yake kutumia pesa za 2015/2016 itakarabati barabara  kilomita 500 katika maeneo hayo.

Wakati uo huo, wakaazi hao waliiomba Serikali ya Kaunti ya Kisii kulikarabati soko la Marani haraka ili shughuli zao ziwe zikiendeshwa kwenye vibanda ndio wakinge mvua.

Soko hilo lingali linaendelea kukarabatiwa, shughuli ambayo wakaazi hao wameiomba kuharakishwa kwa haraka maana hua wananyeshewa wakiwa sokoni  kunaponyesha.