Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wa Mji wa Kisii wanaendelea kusherehekea  matunda ya ugatuzi, baada ya serikali ya kaunti ya Kisii kuendelea kuinua viwango vya maendeleo hasa kuweka mataa katika sehemu mbalimbali ili kuendelesha biashara hata wakati wa usiku.

Akiongea siku ya Jumatano katika mkahawa mmoja mjini Kisii, Gavana wa kaunti hiyo James Ongwae alisema serikali yake inaendelea kufanya kila wawezalo ili kuinua viwango vya maendeleo ya kaunti yake.

“Hadi sasa tumeweka zaidi ya mataa 300 katika mji huu ili kuendeleza biashara katika mji huu hasa wakati wa usiku,” alihoji Ongwae.

Baadhi ya sehemu ambazo zimefaidika na mradi huo ni soko la Daraja Mbili ilioko mji wa Kisii, Mwembe tayari na Jogoo.

Kutokana  na mataa hayo yanayofahamika kama mulika mwizi, uhalifu umepungua kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na hapo awali ambapo watu hutembea usiku bila kuogofya maisha yao.

Baadhi ya wanabiashara waliiongea na mwadishi huyu wamesema wamefaidika pakubwa  kwa kuwa siku hizi hufanya biashara zao hata wakati wa usiku.

“Siku hizi huwa tunafanya biashara hata wakati wa usiku bila kuogopa kwa kuwa kuna usalama wa kutosha,” alisema Erick Kengere, mwanabiashara wa nguo.

Kwingineko wakazi hao wameombwa kushirikiana na serikali ya kaunti kwa maendeleo Zaidi, na kuomba mradi huo wa mataa kuwekwa kila mahali.

Kwa upande wake naibu Gavana wa Kaunti Joash Maangi, wataendelea  kufanya kazi kwa pamoja na kufanya kaunti ya Kisii kuhorodheshwa kuwa bora.