Wakaazi wa Mombasa wakishirikiana na mashirika ya kijamii wametishia kuelekea mahakamani kupinga kupitishwa kwa bajeti ya serikali ya Kaunti.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya wakaazi hao kutofautiana na jinsi makadirio ya bajeti yalivyowasilishwa kwao, kwa kusema kuwa walipewa muda mdogo wa kupitia na kuichanganua bajeti hiyo.

Wakiongozwa na Lucas Fondo, wakaazi hao walidai kuwa serikali hiyo imekiuka katiba inayoagiza makadirio ya bajeti kupewa wananchi kwa kipindi cha siku saba ili waweze kuipitia na kutoa mapendekezo yao.

“Tatamuandikia barua msimamizi wa bajeti kusitisha kutoa pesa hizo hadi pale sheria na mahitaji yetu yatakaposikizwa na kupitishwa,” alisema Fondo.

Fondo alisema kuwa kama wakaazi wamejawa na wasisiwasi baada ya wawakilishi wadi wa bunge la kaunti kukosa kufika kwenye kikao cha Jumatatu kilicho andaliwa katika ukumbi wa Tononoka.

Akiwateta wawakilishi hao, mwanakamati katika kamati ya fedha amesema kuwa wawakilishi hao wamekuwa kwenye kikao maalum kujadili jinsi bajeti hiyo itawekwa wazi kwa wananchi.