Wakaazi wa Kijiji cha Odiyo Wang’e kilichoko Kaunti Ndogo ya Muhoroni wametakiwa kujenga choo ili kuboresha mazingira yao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hayo yalisemwa Alhamisi na mwakilishi wa Afya wilaya ya Muhoroni, Elizabeth Angoro ambaye alikuwa akiwahutubia wananchi katika shule ya St Gabriel Academy.

Angoro alisema kuwa hatua hii itasaidia wakazi kupunguza hatari za kuambukizwa na magonjwa yanayotokana na mazingira chafu.

Kwenye kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na watawala wa eneo hilo wakiwemo manaibu wa chifu, viongozi wa jamii (Community Elders) pamoja na wawakilishi wa elimu ya uma katika jamii, ilibainika kuwaneo hilo hazina choo.

 “Amri imetolewa na wizara ya afya katika Kaunti zima ya Kisumu kwamba kila boma, shule, kanisa na soko kuchimba choo ili kuimarisha afya ya jamii,” alisema Angoro wakati wa mkutano huo.

Wawakilishi wa jamii pamoja na watawala waliombwa kuandaa vikao kila mara ili kuwaelimisha wananchi kuhusu amuhimu wa mazingira.

 Wananchi pia waliombwa kujitokeza katika mikutano ya baraza za watala ili kujuzwa mambo mengi.