Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa wadi ya Sensi kaunti ya Kisii wako na kila sababu ya kutabasamu baada ya mwakilishi wa wadi hiyo, Nyagaka Ochong’a kuwahakikishia wakaazi wa wadi hiyo kuwa ataweka mradi wa maji katika eneo la Nyakeiri hivi karibuni.  

Akizungumza siku ya Alhamisi katika hafla ya mazishi ya Monyenche Nyakundi yaliyoandaliwa katika shule ya upili ya wavulana ya Nyakeiri, mwakilishi huyo alisema tayari wamemaliza mikakati ya kuweka mradi wa maji hayo ili wakaazi wa eneo hilo kunufaika zaidi.

“Serikali yetu ya kaunti ya Kisii ilishirikiana nami kwa kuwekwa mradi wa maji hapa katika eneo la Nyakeiri ili wakaazi wale ambao wamekuwa wakitafuta maji kwa kutembea safari ndefu wapumzike kidogo. Sasa watakua wanachota maji hapa karibu,” alisema Nyagaka Ochong’a.

 “Maji hayo yatawekwa kando mwa shule ya msingi ya Nyakeiri eneo lililo katikati kwa wakaazi wa eneo la Chimo, Nyagoto, nyachogu na Sombogo,” aliongezea Nyagaka.

Ukosefu wa maji umekuwa ukiwasumbua watu wengi wa eneo la Sensi jambo ambalo limepata suluhu kupitia mwakilishi wa eneo hilo, ambaye alisema wakaazi wa eneo hilo hawatasumbuka tena kwa kukosa maji.  

Mwakilishi huyo pia aliombawakaazi kuwa watulivu na kusema atafanya maendeleo mengi zaidi katika eneo hilo kabla ya uchaguzi ujao.

“Wakati serikali za ugatunzi zilianzishwa, hatukuwa na kila kitu lakini mtoto huanza kutembea polepole.  Sisi tulianza kutembea polepole lakini tutatimiza tuliyoyaanza. Nawaomba muwe na subira,” alisema Nyagaka.