Wakaazi wa Wadi ya Nyatieko, kaunti ya Kisii wana kila sababu ya kutabasamu baada ya gavana wa kaunti hiyo ya Kisii James Ongwae kuwaahidi kuweka maji katika soko la Nyatieko.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano katika eneo eneo la Nyabonge, karibu na soko hilo ya Nyatieko, wakaazi hao walisema wako na furaha baada ya gavana Ongwae kutembelea eneo hilo jana na kusema kwa siku chache sijazo watakuwa wamepata maji katika eneo hilo.

Gavana Ongwae alikiri kuwa serikali yake imepanga kuweka maji katika nyumba za wananchi wote wa kaunti hiyo, huku akisema sharti soko zote zilizoko kwa kaunti hiyo kuunganishiwa mradi huo wa maji kwanza.

“Nitaweka maji katika eneo hili la Nyatieko karibuni, na kijana mmoja aajiriwe ambaye atakuwa akifanya shughuli hizo za kupeana maji katika eneo hili,” alisema gavana Ongwae.

“Tunahitaji siku sijazo mwananchi wa kaunti yangu wasisumbuke kwa maji na serikali yangu tayari imeweka mikakati kabambe ya kuweka maji katika nyumba za wananchi wa kaunti hii, tunataka kufanya maendeleo zaidi kwani mlitutuma tufanye maendeleo,” aliongezea Ongwae.

Wakaazi hao walishukuru serikali ya kaunti kwa miradi imeanzisha kwa wakati huu.

“Tunasema asante kwa serikali ya Gavana Ongwae kwa kusema maji yatawekwa katika eneo hili la Nyatieko, kwa sababu tunasumbuka kwa kukosa maji na huenda sasa tupigie kwaheri ukosefu wa maji,” alisema Lydiah Moraa, mkaazi.

“Serikali ya kaunti yetu imeonekana kufanya kazi sasa na tunamwombea gavana kuendelea kufanya maendeleo zaidi kama wananchi wa kaunti hii ili tufurahie matunda ya ugatuzi,” alisema Ezra Omwango, mkaazi mwingine.