Wakaazi wa wadi ya Tabaka iliyoko eneo bunge la Mugirango kusini kaunti ya Kisii wameiomba serikali kuweka lami kutoka eneo la Tabaka kuelekea eneo la Bomware wanakotoa mawe ya kuchonga na kutengeneza vinyago.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano wakaazi hao walisema kuwa watalii wanapozuru eneo hilo husumbuka sana na matope na kuomba serikali kuweka lami katika eneo hilo ili kuwarahisishia watalii usafiri wanaposuru eneo hilo.

Aidha, wakaazi hao wamesema kama serikali ya kaunti ya Kisii inahitaji kujimiarisha kibiashara na kiuchumi sharti itengeneze barabara za eneo ambazo watalii hutembea kama ile ya kutoka tabaka –Nyachenge-Bomware.

“Tunahitaji serikali itengeneze barabara hii ya Tabaka kuja hapa Bomware maana watalii husumbuka sana. Tunaomba wafanye kila juhudi wakarabati barabara hii ili tuweze kuinua uchumi wetu na kujimarisha kimaisha,”alisema Peter Bosire, mkaazi.

Serikali ya kaunti ya Kisii imekuwa ikijulikana kupitia mawe hayo ya kuchonga vinyago.

Wakaazi hao wamemwomba mbunge wa eneo hilo Manson Nyamweya kushughulikia kuwekwa kwa lami katika eneo hilo.

“Tunamwomba mbunge wetu Manson Nyamweya kuweka lami katika eneo hili ili watalii wawe wanatutembelea kila wakati,”alisema Titus Osiemo, mkaazi.