Wakaazi wa Lokesheni ya Mwamonari Wadi ya Sensi Kaunti ya Kisii wamemwomba Mwakilishi wa Wadi hiyo Ochong’a Nyagaka kuweka mchanga barabara aliyoilima hapo mbeleni.
Hii ni baada ya Mwakilishi huyo kulima barabara ya kutoka eneo la Chimo kuelekea eneo la Moyari kwa barabara kuu ya kutoka Marani Miruka.
Wakionga na Mwandishi huyu wa Habari siku ya Jumanne Jioni, wakaazi hao walisema mvua inaponyesha eneo hilo halipitikiki kamwe, jambo ambalo limewakera sana na kumwomba Mwakilishi huyo kuweka mchanga haraka iwezekanavyo.
“Mvua inaponyesha gari haliwezi pita barabara hili ukiona hapo magari yanasukumwa, tunaomba Mwakilishi wa Wadi yetu, aweke mchanga tumalizane naye kiroho safi ili akamilishe shuguli aliyoianza,” alihoji Meshack Kerunda mkaazi wa eneo hilo.
Barabara hiyo imekuwa ikisumbua wakaazi hao wanapopita haswa mvua inaponyesha na kusimamisha shughuli za uchukuzi katika eneo hilo.
Kibarua ni kwa Mwakilishi Nyagaka kuweka mchanga na kuwafurahisha wapiga kura wa eneo hilo kwani wakaazi hao ndio walimkalisha kwenye kiti hicho ili awafanyie miradi kama hiyo.
“Akitufanyia jinsi tunahitaji kwa kulikarabati barabara, basi hatuna budi sisi ila kumrudisha kwenye kiti chake, lakini akiwa anaanzisha mradi bila kukamilisha basi kura si kwake tenai,” alisema Nelson Bosire mkaazi wa Lokesheni hiyo ya Mwamonari.
Wakaazi hao sasa wamesema kuwa wanasubiri kuona mabadiliko na kukamilika kwa mradi huo ulioanzishwa na Mwakilishi Nyagaka ili kurahisisha usafiri wao.