Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi nchini NLC, amesema kuwa zaidi ya wakaazi 3,600 kati ya 4,700 wanaoishi katika Shamba la Waitiki wameanza kulipa ada ya umiliki wa vipande vya ardhi walivyotengewa na serikali kuu.
Akizungumza siku ya Jumamosi jijini Mombasa, Dr Mohammad Swazuri, alisema kuwa kufikia sasa tume hiyo haijapokea pendekezo la serikali ya Kaunti ya Mombasa la kutaka kusimamia malipo hayo.
“Ningependa kuwahimiza wakaazi katika Shamba la Waitiki kuendelea kulipa pesa hizo ili waweze kupata vyeti vyao vya umiliki wa ardhi,” alisema Swazuri.
Hatua hiyo inakinzana na ile ya serikali ya Kaunti ya Mombasa kutaka kusimamia malipo ya ardhi hiyo baada ya bunge la kaunti kuupitisha mswada huo wa malipo.