Mwanariadha Panuel Mkungo aliposhinda mashindano ya Bay Road Race. [Picha/ globalnews.ca]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wa Kaunti ya Taita Taveta walimiminika katika mitandao ya kijamii kuelezea furaha yao kutokana na ushindi wa mwanariadha chipukizi Panuel Mkungo, katika mashindano ya kimataifa yaliyokamilika wikendi iliyopita.Mkungo mwenye umri wa miaka 23 na mzaliwa wa Wusi/Kishamba, alimaliza katika nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha ya EQT Pittsburgh 10 Miler yaliyoandaliwa nchini Marekani siku ya Jumapili.Mashindano hayo yanayoendeshwa na shirika lisilokuwa la serikali la P3R huko Marekani, yanalenga kuchangisha fedha za kuinua riadha, elimu na afya, na huwavutia wanariadha bora kutoka kote ulimwenguni.Licha ya kutoka eneo ambalo halina sifa za riadha, Mkungo aliweza kustahimili ushindani mkubwa kutoka kwa Silas Kipruto, Elkana Kibet and Simion Chirchir waliomaliza katika nafasi za pili, tatu na nne mtawalia. Mkungo alimaliza michuano hiyo ya kilomita 21 katika dakika 47.03.Mkungo alianza kutambuliwa katika Kaunti ya Taita Taveta kama mwanariadha chipukizi mwaka wa 2015 aliposhiriki mashindano ya kila mwaka ya Madoka Half Marathon.Hii ni mara ya nne Mkungo kushinda mashindano ya masafa marefu kimataifa. Amewahi ibuka mshindi katika mashindano ya Miami Half Marathon, Around the Bay Road Race and Mercedes Benz Half Marathon.Ushindi wake ulipotangazwa rasmi, mamia ya wakaazi wa Taita Taveta walituma jumbe zao katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuelezea furaha ya ushindi huo.Mchungaji Godfrey Mwanjulu ambaye aligombea wadhfa wa ubunge eneo la Voi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti alikuwa mmoja wa waliompongeza mwanariadha huyo chipukizi."Congratulations Panuel. We have what it takes to make heroes. (Hongera Panuel. Tunao uwezo wa kuwa mashujaa.),” aliandika Mwanjulu.Wakazi wengine pia hawakusita kuonyesha furaha zao.“Congrats bro, keep up! (Hongera kaka, endelea vivyo hivyo!),” aliandika Lizzy Mwakireti.Naye Eliakim Mwazighe aliandika: “Congrats bro. Kumbe hata sisi tunaweza kuwakilisha.”“Hongera brother…sote tu wakenya.ushindi ni wetu sote,” alisema Hecton Maganga.