Wakaazi wa Wadi ya Gesima, Kaunti ya Nyamira wamehofia maisha yao kutokana na kuaribika kwa daraja linalounganisha barabara ya Nyamokono na Riakworo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongea na Waandishi wa Habari leo Jumatatu asubuhi katika eneo hilo la Nyamokono, wakaazi hao wakiongozwa na aliyekuwa diwani wa eneo la Gesima Julius Nyachio walionyesha hofu yao kutokana na uharibifu huo wakisema kuwa daraja hilo ambalo maji yanapita juu halipitiki kamwe haswa kukinyesha.

Kwa sasa wameiomba Serikali ya Kaunti ya Nyamira kulikarabati daraja hilo kabla maisha ya watu kupotea.

“Watu wengi wameanguka humu ndani ya ya maji yanayofurika kwa nguvu mno wakijaribu kuvuka ng’ambo ile ya daraja haswa watoto wa shule. Imelazimu baadhi ya vijana kuvukisha watu hadi upande ule mwingine,” alihoji Nyachio.

Daraja hilo ambalo hutumiwa na watu wengi zaidi limewazuia wengi wa wakaazi wa eneo hilo kuchelewa kufika kazini mwao kwani wamelazimika kufuata njia zingine mbadala haswa walimu pamoja na watoto wa shule.

“Tunaomba hatua ya dharura ichukuliwe kulikarabati daraja hili kabla maafa yatokee,” alisema Grace Monyenye, mkaazi mwingine wa eneo hilo.