Wakaazi wa Kaunti ya Kisii wamejawa na furaha tele baada ya eneo hilo kupokea mvua iliyokua imeadimika kwa muda wa takribani miezi mitatu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Huku wakiwa wamejawa na furaha wenyeji wa Kaunti hiyo wameelezea matumaini yao ya kupokea mavuno kwa wingi msimu huu licha ya kukawia kwa upanzi.

“Nimefurahi kwa kurejea kwa mvua na nina imani kuwa nitapata mavuno mengi musimu huu” alieleza Moracha, mkaazi na mkulima Kisii.

Baadhi ya wakulima waliokuwa wameshatayarisha mashamba yao wanajiandaa vilivyo kuanza upanzi wa mimea mbali mbali.

Wakulima kutoka eneo hilo wameanza kununua mbegu na mbolea kwa wingi ili upanzi uanze mara moja. Itakumbukwa kuwa eneo la Kisii limeshuhudia kiangazi ambacho si cha kawaida kuanzia mwezi wa Januari mwaka huu hadi hapo jana huku kikiwapa wakati mgumu kwani changamoto nyingi zimekuwa zikiwakodolea macho.

Halikadhalika eneo la Kisii linajulikana kwa utajiri wa mazao kwani mashamba yana rutuba nzuri na hali nzuri ya anga.

Kulingana na mkaazi mwingine Nancy Moraa ana imani kuwa bei ya bidhaa za kilimo kama vile matunda na mboga zitashuka kwa kasi.

“Kwa sasa najua kwamba sitakuwa nanunua bidhaa zingine kwa bei ya juu sana kwani nina imani kwamba bei ya bidhaa hizo muhimu za kilimo kama mboga zitashuka na zitakuwa kwa wingi,” alieleza Moraa.

Hii ni fursa muhimu kwa wakulima kupanda mapema ili kukabiliana na njaa na hali mgumu zinazowakabili kwa sasa.