Wakazi wa eneo la Muchorwe Wilayani Molo wanalalamikia madhara ya pombe haramu baada ya watu wawili kufariki kwenye hadaki la ugemaji wa chang’aa mapema wiki hii.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi hao wamesema licha ya kuwepo kwa maafisa wa polisi wapishi wa pombe hiyo wanaendeleza biashara hiyo katika kituo hicho cha kibiashara huku maafisa wa polisi wakiendelea kudai rushwa.

Wenyeji hao wamesema idadi kubwa ya vijana wameadhirika na pombe hiyo huku wakiitaka serikali kuwahamisha maafisa fisadi ambao wameshidwa kumaliza kero la pombe haramu.

Wakazi hao ikiwemo viongozi wa kidini wamesema maafisa wa usalama katika eneo la muchorwe wamekuwa kikwazo katika vita dhidi ya pombe haramu ambayo inauzwa hadharani.

Aidha wakazi hao wamesema serikali bado haijamchukulia hatua chifu mmoja ambaye ameriportiwa kufanya kazi akiwa mlevi kupindukia.