Wakaazi wa  Mombasa wakiandamana wakilalamikia ukosefu wa usalama na ubaguzi. Picha-Hillary Makokha

Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya viongozi kutoka katika kaunti ya Mombasa siku ya Ijumaa waliandamana mjini Mombasa wakilalamikia ukosefu wa usalama, ubaguzi wa ajiri na utenda kazi mbaya wa serikali ya kaunti ya Mombasa.

Waandamanaji hao wakiongozwa na kiongozi wa Shirika la League of women Forum walipeleka lalama zao kwa afisi ya Rais kupitia kwa mshirikishi wa kanda ya Pwani  Nelson Marwa wakitaka lalama zao zishughulikiwe.

Waandamaji hao wasema kuwa ubaguzi umezidi  sana katika serikali hiyo huku wakisema kuwa mkuu wa utumishi wa uma katika kaunti ya Mombasa ni nduguye Gavana wa Mombasa Hassan Joho.

Masuala mengine ambayo yalitajwa na waandamanaji hao ni kutotumika vizuri kwa pesa za kulipa kodi za mwananchi wa kawaida.

Waandamanaji hao sasa wanaitaka serikali kuu kuchukulia lalama zao kama suala la dharura na hatua za haraka kuchukuliwa.

Waliongeza kuwa wanaitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kupeana stakabadhi zote za kuonyesha jinsi pesa zimekuwa zikitumika na kupeana makataa ya siku 14  katika serikali ya kaunti ya Mombasa maswala yao yawe yametatuliwa la sivyo watachukuwa hatua zingine.