Mbunge wa eneo bunge la Kitutu chache kusini Richard Momoima Onyonka amewaomba wananchi wote wa kaunti ya Kisii kushirikiana na viongonzi kuleta maendeleo.
Akiongea siku ya Ijumaa katika hafla ya mazishi ya Chrisatos Mekenye Omoi yaliofanyiwa katika uga wa shule ya upili ya Marani, Onyonka aliomba wananchi kuunga mkono viongonzi walio kwa uongozi na kushirikiana nao ili kuleta maendeleo zaidi.
“Mimi niko tayari kushirikiana na gavana wetu wa Kisii James Ongwae na viongonzi wote. Nawaomba nanyi mshirikiane na viongonzi hawa ili maendeleo yaweze kunawiri zaidi katika kaunti yetu,” alisema Onyonka.
Wakati huo huo, mbunge wa eneo bunge la kitutu chache Kaskazini Jimmy Nuru Angwenyi aliunga mkono matamshi ya mbunge huyo Richard Momoima na kusema ushirikiano utaleta maendeleo zaidi katika kaunti ya Kisii.
“Sisi sote tukiongea kwa sauti moja na kufanya maendeleo pamoja basi kaunti ya Kisii itasonga mbele kimaendeleo,”alisema Angwenyi.
Hafla hiyo iliuhudhuriwa na viongonzi mbalimbali akiwemo aliyekuwa mbunge wa Kitutu Masaba Walter Nyambati, seneta mteule kaunti ya Kisii Hosea Ojwang’, gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwe na mawakilishi wa bunge ya kaunti ya Kisii na wananchi kwa jumla.
Viongonzi waliokuwa kwa hafla hiyo waliwahakikishia wanachi kuwa watashirikiana kuleta maendeleo Kisii.