Wakaazi mjini Nakuru wametakiwa wajihadhari na wahalifu kwenye mitandao ambao wanalaghai wakenya.
Hayo yalijiri baada ya mfanyibiashara mmoja mjini Nakuru kutekwa nyara na watu waliokutana kwenye mtandao na kujifanya kuwa ni wanunuzi wa gari lake.
Mfanyibiashara huyo Alex Mariera alikutana na watu hao alipokuwa akiuza gari lake kwenye mtandao.
Inaarifiwa walijifanya wateja na wakasafiri hadi mjini Nakuru kuliona gari hilo. Hata hivyo, Mariera alipatikana ameuawa baada ya kwenda kukutana na wanunuzi hao.
Polisi walisema wahalifu enzi hizi wamepiga kambi kwenye mtandao.
“Watu wajihadhari sana, ni makosa sana kwenda kukutana na watu usiowajua peke yako. Hizi biashara za mitandao ama mapenzi ni hatari sana,” afisa mmoja wa polisi Nakuru alisema.