Mwakilishi wa wadi ya Kiamabundu Wilfred Yoge amewaonya wakaazi dhidi ya kuuza mashamba kiholela.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Yoge ambaye alikuwa akiongea katika hafla ya mazishi aliwaomba wakaazi kuwafikiria watoto wao kabla ya kufanya uamuzi wa kuuza shamba.

Haya yalijiri baada ya habari kuibuka kuwa mama ambaye alikuwa anazikwa alikuwa ameuza shamba lake miaka michache kabla ya kifo chake.

Jambo hilo lilileta malumbano makali kati ya walio nunua shamba hilo na watoto wa mwenda zake.

Yoge pia aliwaomba wanao nunua mashamba kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuyanunua.

"Ni vyema unaponunua shamba kufanya utafiti ili ujue mwenye shamba ni nani na kama shamba lenyewe ni halali,” akaomba Yoge.

“Mizozo mingi hutokea wakati aliyeuza shamba amekufa. Huo ndio wakati watu hujitokeza na kukiri kwamba ni wamiliki wa shamba hilo,"  akasema Yoge.

Mwakilishi huyo alisema kuwa mambo kama hayo huleta aibu kwa jamii. 

Kwa upande wake Chifu wa lokesheni ya  Kisii ya kati George Nyamwaka aliwaahidi wakaazi kuwa ataweka sheria itakayosaidia kupambana na kesi za mashamba.