Wakaazi wa kaunti ndogo ya Njoro wameombwa kushirikiana na maafisa wa usalama katika harakati za kupambana na unywaji na upishi wa pombe haramu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Naibu kamishna wa jimbo hilo Mohamed Hassan amesema ushirikiano kati ya wananchi na vitengo mbali mbali vya usalama kutawezesha wilaya hiyo kukabiliana na wale wanaoendeleza biashara hiyo.

Hassan alisema kuwa utawala wa mkoa umefanikiwa kufunga baadhi ya mashimo ambayo upishi wa pombe aina ya chang’aa na kangara unatekelezewa.

Hassan alitazama kuwa hatua hiyo imefaulu baada ya wakaazi kuhusishwa katika oparesheni za mara kwa mara.

Amesema maafisa wa utawala pamoja na polisi wanashirikiana na mamlaka ya kukabiliana na pombe haramu na dawa za kulevya (NACADA) ili kukomesha biashara hiyo ambayo ina madhara makubwa katika jamii.

 Aidha afisa huyo amesema msako utaendelezwa hadi kwenye vilabu ili kuhakikisha pombe ambazo hazijaidhinishwa na halimashauri ya ubora wa bidhaa (KEBS) haziuzwi ili kuepusha eneo hilo na madhara ambayo yameshuhudiwa katika maeneo mengine nchini.