Wakenya wengi wamependekeza adhabu kali kuchukuliwa kwa watakaopatika na hatia ya kuwahusisha wanafunzi wa darasa la nane na upili dhidi ya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa nchini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongozwa na Kiongozo wa vijana katika eneo la Kisauni mjini Mombasa Maxwell Masai, wamesema kuwa ripoti iliyotolewa na baraza la mitihani nchini Knec kuwa baadhi ya maafisa wa baraza hilo na maafisa wa wawili wa polisi kutoka kituo cha polisi cha kaskazini mashariki mwa nchi imeonyesha wazi kuwa wizi wa mitihani ulitekelezwa.

Akizungumza katika eneo la Kisauni mjini Mombasa siku ya Jumanne kwenye mkutano wa wakaazi, Masai amesema kuwa hatua iliyochukuliwa ya kuvunjiliwa mbali kwa baraza la mitihani imeonyesha hatua mwafaka ya kukabiliana na uwizi wa mitihani ya kitaifa na juhuzi hizo zitaimairisha sekta ya elimu.

"Tunaishinikiza serikali kuhakikisha kuwa inawachukulia hatua kali wale watakaopatikana wakiwashirikisha vijana katika maswala ya udanganyifu wa mitahani ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya vyema katika mitihani yao ya kitaifa," alisema Masai.

Kwa sasa wakaazi hao wanapendekeza serikali kuwachukulia hatua za kisheria sambamba na kubuni hatua hali kwa wataopatikana wakiwahusisha wanafunzi kushiriki udanganyifu wa mitihani nchini.