Wakazi wa Soko la Mwala katika kaunti ndogo ya Mwala kaunti ya Machakos wamelalamikia kutokuwa na mahali mbadala pa kutupa takataka, huku wakisema jambo hili limechangia takataka kutapakaa na kuharibu mazingira. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katika mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo, walielezea kuwa wafanyakazi wa kaunti hukusanya takataka hizi katika mahala pamoja pale baada ya siku kadhaa takataka hizi hutapakazwa na mbwa na ndege wanaotafuta chakula. 

Aidha wakazi hawa walielezea kuwa takataka hii inapochelewa kuondolewa huwa kunazuka harufu mbaya inayoadhiri biashara hasaa kwa wanaouza vyakula.

"Hakuna mteja atanunua bidhaa mahali ambapo mazingira yake sio ya kupendeza," alisema, Titus Kioko, mfanyabiashara katika soko hilo.

Isitoshe wakazi hawa wanahofia kuzinduka kwa maradhi yanayotokana na uchafu. 

Wakazi hawa waliitaka serikali ya kaunti ya Machakos kutenga ardhi ambapo takataka itakuwa ikitupwa ili kuhifadhi mazingira.