Wakaazi wa eneo bunge la Nakuru mjini mashariki na hasa wadi ya Kivumbini wametakiwa kujivunia kituo cha afya cha akina mama kujifungua kilicho mtaa wa Bondeni. Afisa msimamizi wa kituo hicho cha afya Salome Gachathi katika mahojiano Jumatatu, alisema wakaazi wanafaa kujivunia kituo hicho kwani kina manufaa si haba.
Isitoshe alidokeza kuwa tangu kituo hicho cha kujifungua Kwa akina mama cha Bondeni kimepiga hatua tangu kiwe chini ya usimamizi wa serikali ya kaunti ya Nakuru. "Ningependa kusema kuwa tumepiga hatua katika kituo hiki na ni kutokana na juhudi za kaunti na ugatuzi Kwa jumla," Gachathi alisema.
Hata hivyo, alitoa wito Kwa serikali na wahisani kushirikiana ili kuhakikisha kuna uimarishwaji wa huduma.