Wakaazi wa Nakuru wametakiwa kuwekeza katika biashara ya nyumba za kupanga ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la watu wanaohamia mjini humu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Waziri wa nyumba na mipango katika jimbo la Nakuru Rachael Maina alisema kuwa Nakuru inakumbwa na tatizo kubwa la uhaba wa nyumba za makaazi tatizo ambalo alisema linasababishwa na ukuwaji kwa haraka wa mji na ongezeko kubwa la idadi ya watu.

Akiongea Ijumaa alipokagua nyumba za serikali katika mtaa wa Bondeni,Maina aliwata wakaazi wenye uwezo kutumia fursa hii ili kujiimarisha kimaisha kwa kujenga nyumba za kupanga.

“Mji wetu wa Nakuru unakua kwa kasi sana nah ii imefanya watu wengi sana kuingia mjini Nakuru lakini sekta ya ujenzi imesahau kuwekeza katika ujenzi wa makaazi mapya nah ii imesababisha upungufu wa nyumbaza kupanga.Hii ni fursa nzuri kwa watu walio na mashamba karibu na mji kuwekeza katika nyumba za kupanga maanake kuna soko la tayari,” alisema Maina.

Maina alisema kuwa wizara yake iko tayari kushirikiana na wale wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuwapa mipango ya ujenzi inayofaa.

“Tutasaidiana na wale wote ambao wamejitolea kutusaidia kutatua tatizo la uhaba wa nyumba mjini Nakuru na tuko tayari kuharakisha  shuguli za kuthibitisha mipango yao ya ujenzi ili waweze kuanz shuguli za ujenzi mara moja,” alisema.

Wakati uohuo Maina alisema kuwa serikali itaanza shuguli ya kukarabati nyumba zake zote ili ziweze kufikia viwango vya kisasa.