Wakaazi wilayani Nyamache kaunti ya Kisii wametishia kuandamana kulazimisha serikali kuwawekea matuta katika barabara ya kutoka kisii kuelekea kilgoris.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya watu wawili waliokuwa kwa pikipiki kugongwa na gari aina ya Nissan na kufariki papo hapo. 

Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa dereva wa gari hilo alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi. Waendesha pikipiki wenye hamaki walichoma gari lililosababisha ajali hiyo.

Wakizungumza hii leo katika eneo hilo la Nyamache wakaazi hao wakiongozwa na Ken Omariba walisema hii si mara ya kwanza watu kufariki kupitia ajali za katika barabara hiyo kwani hakuna matuta ambayo yamewekwa kupunguza mwendo wa kasi.

“Tutapanga maandamano ikiwa serikali haitaitikia wito wetu na kutuwekea matuta kwa wiki moja ijayo,” alisema Omariba.

“Wengi wamepoteza maisha kupitia ajali zinazofanyika katika barabara hii na hatutaendelea kuruhusu visa vya aina hii kuendelea kila wakati,” alisema Kevin Onyancha, mkaazi mwingine.