Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baada ya wakaazi wa baadhi ya maeneo ya kaunti ndogo ya Rongai kulalamikia ukosefu wa machifu kwenye maeneo ya Magare, Legetio na Burgei, sasa maeneo hayo yatapata machifu kabla ya Jumanne wiki ijayo.

Akidhibitisha hayo Jumapili hii, Naibu Kamishina wa Rongai David Koskei amesema kuwa, tayari amefanya usajili na kupata machifu ambao watashughulikia maslahi ya wananchi na kutatua mizozo ambayo imekuwa ikishuhudiwa kwenye maeneo hayo.

“Tayari tumewapiga msasa wote watakaoandikwa kabla Jumanne wiki ijayo kuwa machifu,” alisemaKoskei.

Aliongeza kwakusema kuwa, shughuli ya kuleta machifu wapya imekawia kwani ilawalazimu kuzingatia swala la jinsia na viwango vya elimu.

“Shughuli hii kidogo ilichukua muda kwa sababu kuna matakwa mengi ambayo yanafaa kuzingatiwa lakini tunashukuru maanake sasa tuko tayari kuyatekeleza,” alisema Koskei.

Swala hili limejiri mwezi mmoja baada ya wakaazi Wa kutoka maeneo hayo kutishia kufanya maandamano wakilalamikia kusahaulika.