Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi kutoka serikali ya kaunti ya Nakuru pamoja na viongozi wa kidini Jumamosi walifanya maandamano ya amani katika barabara za mji wa Nakuru katika kuwakumbuka maafisa wa KDF walioaga dunia.

Ni msafara ulioshia katika bustani ya Nyayo mjini Nakuru ambapo mishumaa iliwashwa katika kuonyesha heshima kwa maafisa hao wa kdf walioaga.

Wakiongozwa na gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua , viongozi hao walihimiza serikali kutolegeza kamba katika vita dhidi ya ugaidi.

Aidha, walihimiza wakenya wote kuuungana pamoja wakati huu ambapo kenya inapitia wakati mgumu na pia kuunga juhudi za serikali katika kupambana na ugaidi.

Kwa upande wake Sheikh Naoro Hamisi ambaye ni Kiongozi wa dini ya kiislamu alikariri kwamba wakati umewadia kwa wakenya kufanya kazi ka pamoja na kuungana bila ya kuzingatia tofauti zao za kidini.

ni vyema kuashiria hapa kuwa vingozi balibali wamekuwa wakituma risala zao za rambirambi kwa jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao kuytokana na shambulizi lililotekelezwa dhidi ya wanajeshi wa kdf huko somalia.