Mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki mjini Mombasa wanatarajiwa kuungana na wenzao ulimwenguni kuadhimisha ibada maalum ya mkesha wa kufufuka kwake Yesu Kristu usiku wa siku ya Jumamosi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ibada hiyo inaambatana na Jumapili ya Pasaka ambayo waumini hukumbushwa mateso ya Yesu Kristu kabla ya kufa na kufufuka kwake kulingana na imani ya dini hiyo.

Akizungumza siku ya Jumamosi mjini Mombasa, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mombasa Askofu Martin Kivuva, aliwasihi Wakirstu kuzingatia mafundisho ya dini wakati wanaposheherekea Pasaka pamoja na kuwakumbuka wasiojiweza.

“Waumini wa katoliki wataadhimisha ibada maalum ya kesha ya pasaka siku ya Jumamosi ya kuamkia Jumapili ya Pasaka, na pia tunawahimiza waumini na Wakenya kwa jumla kuzingatia mafunzo ya dini na kuwasaidia wasiojiweza,” alisema Askofu Kivuva.

Askofu Kivuva aliwarai Wakatoliki na Wakenya kwa jumla kuhakikisha kuwa wanaliombea taifa hili ili kuepukana na masaibu na siasa za chuki wakati taifa hili linapokaribia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kiongozi huyo wa dini aliwahimiza Wakenya kuzidi kudumisha amani pamoja na kujitenga sna iasa zisizokuwa na msingi wowote.