Wakazi wa wadi ya Elementaita, eneo bunge la Gilgil wanalalamikia hali mbaya ya barabara katika eneo hilo kufuatia mvua inayoendelea kunyesha.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi hao wanamlaumu mwakilishi wa wadi hio Moses Nd'ungu kwa kufeli kurekebesha hali ya barabara katika wadi yake.

"MCA wetu hajafanya lolote kuunda barabara zetu. Sasa tunateseka maana imekuwa ngumu hata kwa magari kufika hapa," alisema Marvin Njehia.

"Ukitembea kwa hii barabara utapata magari mengi yakiwa yamekwama, na ikifika wakati wa kuomba kura watakuja hapa kutuomba. Hii barabara ingerekebishwa kabla mvua ianze. Sasa sijui sisi wakazi tutatumia barabara ipi," aliongeza Joe Kageni.

Wakazi hao wanasema kuwa hata baada ya kutoa malalamishi yao kwa afisi ya mwakilishi huyo hakuna hatua yeyote imechukuliwa.

"Tumekuwa tukienda kwa ofisi yake kupeleka malalamishi na kila mara tunaahidiwa kuwa hii barabara itarekebishwa," alisema Susan Gathoni.

Juhudi za kuongea na mwakilishi wa wadi hii ziligonga mwamba.