Wakaazi wa eneo la Kisauni wamelalamikia hali mbaya ya mabomba ya majitaka katika eneo hlio ambayo wanasema kuwa mengine yametoboka na kumwaga maji hayo barabarani jambo ambalo kulingana nao limesababisha maeneo mengi Kisauni kuwa na harufu mbaya.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na mwanabiashara mashuhuri Ali Mbogo siku ya Jumatano, wakaazi hao sasa wametishia kufanya maandamano ya amani hadi kwa gavana wa kaunti hiyo Hassan Joho ili kuwasilisha malalamiko yao kwa serikali ya kaunti.

Wakaazi hao walisema kuwa wamejaribu kumfikia mbunge wa eneo hilo Rashid Bedzimba ili ajaribu kutafuta suluhu ya kudumu lakini hawajafua dafu.

“Tumejaribu tumwone mbunge ili tumweleze vile hali imekuwa mbaya Kisauni, lakini wale ambao wamemzingira hawaturuhusu kumfkia,” alisema Rashid Kombo ambaye pia ni mkaazi wa eneo hilo.