Wakaazi wa Tayari, kwenye Wadi ya Molo, wamelalamikia ukosefu wa maji katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi hao walisema kuwa eneo hilo limeshuhudia ongezeko la watu na hivyo kisima kimoja walichokuwa wakikitegemea hakiwezi kukithi mahitaji yao.

"Mtaa huu sasa una watu wengi zaidi na ukienda kuteka maji kwa kisima utapata foleni ndefu sana. Kupata maji imekua balaa kwa kuwa kiza hutupata tukisaka maji," alisema Mary Munene, mkaazi.

Kwa sasa wakaazi hao wamemtaka Mbungu wa Molo Jacob Macharia na mwakilishi wa Wadi ya Molo Joseph Ngugi kuwatafutia njia mbadala ya kupata maji.

"Tunamuomba mbunge wetu na mwakilishi wa wadi washughulikie swala hili kwa dharura," alisema Stella Nyaboke, mkaazi.