Baadhi ya wanachi jijini Mombasa wanaunga mkono kauli ya raisi kuwataka magavana kuwa na malengo ya kujisimia kifedha katika kaunti zao badala ya kungojea pesa kutoka kwa hazina ya serikali kuu.
Wakngumza na mwanahabri huyu siku ya Alhamisi, Salim Ahmed, mkazi wa Likoni, alisema kuwa serikali za kaunti ziko na rasilimali nyingi zilizosaulika na iwapo zitaimarishwa basi serikali za kaunti zitaweza kujikimu kifedha.
Aidha, amewataka magavana kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uchumi na pato la kaunti badala ya kusubiri mgawo kutoka kwa serikali kuu.
Kauli hii inajiri baada ya raisi Uhuru Kenyatta kuzitaka serikali za kaunti kuwajibika katika kutafuta fedha zitakazo kimu mahitaji ya wananchi wao badala ya kusubiri pesa kutoka kwa serikali kuu.
Raisi alisema lazima magavana watoke kwenye hulka ya kupewa pesa kutoka kwa serikali na badala yake wazingatie kukuza rasilimali zao ili wapate ushuru.
Aliongeza kuwa serikali za ugatuzi ziliwekwa ili kaunti ziweze kushughulikia maswala ambayo wanaona serikali kuu imesahau na sio kurudi kuililia serikali hio kila kukicha.
Wakati huo huo Uhuru alikanusha madai yanayoendelea kuenezwa na magavana hasa wa upande wa upinzani kuwa serikali kuu imepuuzilia swala la utoaji wa fedha ambapo wanatoa kwa mkato mkato.