Kinara wa Nasa Raila Odinga.[Osman Suleiman]Kinara wa Muuungano wa Nasa Raila Odinga amewataka wakazi wa Mombasa kutumia bunge la wananchi kushinikiza uongozi duni wa serikali ya Jubilee.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumapili wakati wa uzinduzi wa Bunge hilo jijini Mombasa,Raila alisema kuwa wakazi wa Mombasa wamengwa kwa muda mrefu na serikali ya  Jubilee hasa katika maendeleo.

Alilitaja bunge la wananchi kama litakalo wasaidia watu wa Mombasa kupitisha miswaada yenye manufaa kwao na ambayo itazidi kuboresha kaunti nzima ya Mombasa.

Raila amewataka wakazi wa Mombasa kutumia bunge la wananchi katika kupinga unyanyasaji,ukoloni mambo leo na kupinga kuhamishwa kwa utendakazi wa bandari ya Mombasa hadi Naivasha.

Wakati huo huo Odinga ameitaja serikali ya Jubilee kama isiyoheshimu katiba ya nchini na wanapitisha miswaada isiyokuwa na manufaa kwa wakenya.

Aidha,Raila ameshikilia kuwa alishinda uchaguzi wa Agosti nane na anastahili kuapishwa kuwa raisi wa taifa hili na kusisitiza kuwa msimo wake wa kuapishwa Januari 30 bado ungalipo na mipango iko tayari ya kumuapisha.