Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kila mkazi katika kijiji cha Anyiko kwenye Kaunti Ndogo ya Muhoroni ametakiwa kuchimba choo nyumbani mwake.

Agizo hili linalenga kuimarisha afya na mazingira masafi katika makazi yao. Afisa wa mazingira kutoka katika wizara ya afya ya Kaunti hiyo ndogo, Bi Monica Achieng aliwaonya wakazi ambao hawana vyoo manyumbani mwao na ambao wanatumia misitu kuenda haja kubwa kwamba watakabiliwa na sheria za afya na mazingira.

''Uchafuzi wa mazingira unaotokana na kinyesi huchangia magonjwa mbalimbali na ni hatari kwa afya ya uma kwa hiyo ni muhimu kila mmoja awe na choo kwake,'' alisema Achieng.

Achieng alisema haya akiwa katika mkutano wa baraza la mkuu wa kijiji hicho ulioandaliwa mnamo siku ya Jumatatu.

Katika baraza hilo lililoandaliwa mahususan kuwahamasisha wakazi kuhusu umuhimu wa mazingira masafi, makataa ya miezi mitatu yalitolewa kwa kila mtu asiyekuwa na choo nyumbani mwake kuhakikisha amemaliza kuchimba na kujenga choo kwake.

''Amri imetolewa na wizara ya afya katika kaunti nzima kwamba kila mtu awe na choo nyumbani mwake kabla ya msako kuanzishwa wakati makataa ya miezo mitatu kumalizika.

Agizo hili limekuja wakati ugonjwa wa kipindupinda inahofia kuvamia Kaunti ya Kisumu.

Duru za kuaminika zilisema kuwa baadhi ya watu kijijini hapo hutegemea kwenda haja kubwa kwenye vyoo vya shule zilizoko karibu nao.