Wakazi wa Kaunti ya Nyamira wameombwa kushirikiana na wawekezaji wa kigeni ili kuimarisha kilimo na kustawisha maendeleo.
Akihutubia wananchi kwenye hafla yakuadhimisha siku ya chakula duniani kule Rigoma siku ya Ijumaa, Kamishna wa Kaunti ya Nyamira Bi Josphine Onunga alisema kuwa ili kaunti hiyo kustawi, sharti wakazi washirikiane na wawekezaji wanaotaka kuekeza nchini.
Onunga alisema kuwa ushirikiano katika maendeleo waweza imarisha sekta ya kilimo nchini.
"Ushirikiano katika maendeleo waweza imarisha sekta ya kilimo nchini, na ninawasihi vijana humu Nyamira kukumbatia miradi iliyoanzishwa na serikali ya kitaifa ili kuimarisha mapato yao,” alisema Onunga.
Kamishna Onunga aidha aliwaonya wakazi dhidi yakuketi nakungoja kupokea misaada kutoka kwa serikali.
"Nawaonya wananchi dhidi ya mazoea yakukaa tu nakungoja serikali kuwapa misaada. Wakazi kama hao hawatapewa nafasi yakuendea na tabia hiyo Nyamira,” alisema Onunga.