Wakazi wa mtaa wa Bondeni mjini Nakuru wanaomba serikali ya kaunti kushughulikia mtaa wa Ziwani ambao uko mkambala na mtaa huo wao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mtaa wa Ziwani ambao ulikuwa mali ya shirika la zamani la reli (Kenya Railways) ulibaki ukiwa wakati watu walokuwa wakiishi humo walifurushwa.

“Wakaaji walikuwa wanavamiwa usiku na mabati ya paa za nyumba zao kung’olewa. Kitendo ambacho iliwafanya wahame mmoja,” alisema Miriam Ngima, mkaazi wa Bondeni.

“Kuhama kwa watu hawa kimekuwa chanzi cha wizi hapa kwetu kwani yale manyumba yaliyobaki yanatumiwa na wahalifu kujificha,” aliongeza Miriam.

Hata hivyo uhalifu huu umepungua tangu mahala pale pawekwe chini ya ulinzi. Kuna madai kuwa uwanja huo ulinunuliwa na serikali ya kaunti ya Nakuru na haijabainika serikali ina mpango gani kuhusu eneo hilo.

“Mahala hapa panastahili patengenezwe steji ya matatu. Hata wale wachuuzi wanaofurushwa huko mjini wanastahili kujengewa hapa kama ilivyofanyika huko Nairobi upande wa Muthurwa,” alisema Boniface Omware ambeye pia ni mkaazi wa Nakuru.

Omware anaamini kwamba eneo hilo likijengwa steji na soko, mtaa wao wa Bondeni utajengwa nyumba nzuri kinyume na wakati huu ambapo hauna nyumba za kupendeza, na kuwa katika hali mbaya.

“Bondeni saa hii ni kama kitongoji duni lakini, ziwani kukijengwa hapa, wamiliki wa ploti hapa watalazimika kujenga majengo ya kisasa,” aliongezea Omware.