Wakazi wa maneo ya Jogo na Coke wamepongeza hatua ya kaunti ya Kisii kukamilisha ukarabati wa barabara zinazounganisha kaunti na kuingia mjini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Shughuli ya ukarabati huo ilianza mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015 na umekuwa ukiendelea kwa miezi mitatu sasa na mojawapo ya barabara ambazo zimekuwa zikisumbua watumiaji ni ile inayotoka njia-panda ya Jogo na kuelekea kwenye kiwanda cha kutengeza soda cha Cocala na ile inayolekea Riomakondo.

Iyo ilikuwa miongoni mwa ahadi za gavana wa Kaunti ya Kisii Bwa. James Ongwae alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye kongamano la Uongozi Bora na Ugatuzi juzi kuwa atahakikisha kuwa miundomsingi ya kaunti ya Kisii inaboreshwa na haswa barabara zote ambazo zimekuwa kero kwa wananchi na wakazi wa Kisii kwa jumla.

Barabara hizo mbili zilianza kulainishwa juzi baada ya mchanga aina ya ‘Muramu’ kumwagwa na kukaa kwa zaidi ya wiki tatu huku mwanakandarasi aliyejukumika kutekeleza shughuli hiyo akingojea kunyesha kwa mvua.

Hata hivyo wakazi hao wameiomba serikali ya kaunti kutafuta mchanga wa kudumu ambao hautawasumbua wakati huu wa msimu wa mvua nzito inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini, Kisii ikiwa mojayapo kwani ‘Muramu’ hudumu kwa muda mfupi.