Wakazi wa Kisii wameombwa kuzingatia usafi ili kujikinga na maradhi yanayoenezwa na uchafu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea hii leo katika eneo la Gekomu, mtaa wa Mwembe, mhudmu wa afya ya Jamii Kepha King’oina alisema kuwa kudumisha usafi ni njia moja ya kuepukana na magonjwa.

“Serikali yetu imeweka mikakati ambayo inasaidia kuimarisha usafi; ni jukumu letu kufanya kazi pamoja na serikali ili kurahisisha shughuli hiyo,” akasema King’oina.

King’oina aliwaomba wakazi kuweka uchafu panapostahili ili uchafu huo kuchukuliwa na gari la takataka kwa wakati unaofaa.

 “Nawaomba watu wote kushirikana ili kusaidia kudumisha usafi,” akasema King’oina.

Kwingineko amewaomba wakazi hao kuwa waangalifu kwa chakula zinazopikwa katika mji wa Kisii na kuwaomba wanaopika chakula hizo kuzingatia usafi.

"Si vizuri kukula chakula ovyoovyo hasa zina zopikiwa nje. Ni vizuri kukula chakula ambacho unauhakika kimetayarishwa na mtu ambaye anazingatia usafi," akahoji Kingoina.

Haya ni kutokana na ugonjwa wa kipindupindi  ulioripotiwa katika kaunti nyingi hapa nchini.

 “Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha kuwa chakula anayoikula imetayarishwa kwa njia safi. Jambo hili litatusaidia kujikinga na magonjwa,”akaongeza King’oina.