Wakaazi wa Mishomoroni eneo bunge la Kisauni watanufaika ki usafiri wakati ujenzi wa barabara ya lami maeneo ya mwisho wa lami itakapokamilika.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ujenzi huo unalenga kukarabati barabara hiyo ambayo huwa katika hali mbaya wakati mvua inaponyesha.

Akizungumza alipokuwa akikagua barabara hiyo siku ya Ijumaa alipowahutubia wananchi mwisho wa lami kuekekea Nguu Tatu na Mwakirunge, Mbunge wa kisauni Rashid Bedzimba alimshukuru gavana wa Mombasa Ali Joho kwa kuanzisha mradi huo.

“Ujenzi huu utakaoanza hivi karibuni ni kwa niaba ya ndugu yangu kipenzi gavana Joho. Twaipenda sana Kisauni na maendeleo ni lazima tuwafanyie wakaazi," alisema Bedzimba.

Mradi huo utakua wa afueni kubwa kea wakazi wa eneo hilo la Mishomoroni, ambao wamekuwa na wakati mgumu kutumia barabara hiyo mbovu.