Baadhi ya wakazi mjini Mombasa watakosa maji kwa mda kuanzia siku ya Jumatatu baada ya kituo cha kusambaza maji cha Baricho kufungwa kwa mda ili kikarabatiwe.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana mkurugenzi wa kampuni ya maji mjini Mombasa Sara Lang'ati, usambazaji maji utasitishwa kwa mda ili kituo hicho kikarabatiwe pamoja kusafishwa.

Lang'ati ameyataja maeneo ya Kiembeni, Nyali, Kongowea, Kisauni na Mshomoroni kama yatakayoathirika na uhaba huo wa maji na akawataka wananchi kuwa na subira wakati wanapotekeleza ukarabati huo kwani ukarabati huo hautachukua mda mrefu.

"Tunapitia changamanoto kwa sasa ya ukosefu wa maji safi kutokana na kuharibika kwa bwawa la Baricho linalosambaza maji Mombasa lakini shughuli hiyo inaendelea kwa sasa na hivi karibuni maji yatasambazwa," alisema afisa huyo siku ya Jumatatu afisini mwake.

Haya yanajiri huku wakazi wa Mtopanga eneo la Kisauni wakilalamikia uhaba wa maji kwa miezi mitatu sasa.

Picha: Wakazi wa Mombasa wakisubiri maji licha ya kuwa na changamoto katika mabomba ya kusambaza maji Mombasa.