Wakazi wa kaunti ya Nyamira wamehimizwa kujitokeza kupimwa ugonjwa wa sukari kama njia mojawapo ya kukabiliana na hatari ya ugonjwa huo. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubu kikao cha wanahabari mapema Jumanne, katibu wa wizara ya afya Douglas Bosire alisema kuwa utafiti unaonyesha kuwa wakazi wengi kwenye kaunti ya Nyamira hawajitokezi kupimwa msukumo wa damu, akiongeza kusema kuwa serikali ya kaunti hiyo kwa ushirikiano na hospitali kuu ya Kenyatta zitakuwa na kliniki tamba cha matibabu ya bila malipo Jumamosi tarehe 14.

Aidha, aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupimwa ugonjwa huo, kwa kuwa itawawia rahisi kupata matibabu ya mapema iwapo watakuwa na ugonjwa huo. 

"Nawaomba wananchi wachukue jukumu la kupimwa sukari kwa kuwa siku hizi hata watoto huathirika sana na ugonjwa wa sukari," alihimiza Bosire.