Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi wa eneo bunge la Nyaribari Masaba wana kila sababu ya kutabasamu baada ya mbunge wa eneo hilo Elijah Moindi kuwahakikishia kuwa ataweka mradi wa maji katika maeneo mbalimbali katika eneo bunge hilo.

Akiongea siku ya Jumatatu wakati alikuwa na vikao mbalimbali vya bunge katika eneo bunge hilo ili kukusanya yale wananchi wanamhitaji awafanyie, mbunge huyo aliahidi kuweka mradi wa maji katika sehemu mbalimbali ili wakazi wa eneo hilo waweze kunufaika zaidi.

“Kupitia hazina ya ustawi ya maeneo bunge, maji yatawekwa kila mahali hivi karibuni ili wakazi wale ambao wamekuwa wakitafuta maji kwa kutembea safari ndefu wapumzike kidogo. Mtakuwa mkiteka maji karibu na mnapoishi. Nimekuja na timu nzima ya 'CDF' ili tupige hesabu ya yale mnahitaji,” alisema Moindi.

Ukosefu wa maji umekuwa ukiwasumbua wakazi wengi wa eneo bunge la Nyaribari Masaba jambo ambalo limepata suluhu kupitia mbunge wa wa eneo hilo, ambaye alisema wakazi wa eneo hilo hawatasumbuka tena kwa kukosa maji akiwa mamlakani.

Mbunge huyo pia aliomba wakazi kuwa watulivu na kusema atafanya maendeleo zaidi katika eneo bunge hilo kabla ya uchaguzi ujao ili kuwaridhisha kimaendeleo.

Aidha, mbunge huyo aliahidi kukarabati baadhi ya barabara zile zimearibika katika eneo hilo ili kurahisisha uchukuzi jinsi aliovyoombwa na wakazi wake.

“Ifikapo 2017 mtapata nimewafanyia maendeleo kikamilifu maana mlinichagua niwafanyie maendeleo,”aliongeza Moindi.