Zaidi ya wakaazi 300 kutoka eneo la Weseges, Subukia katika jimbo la Nakuru Jumanne walinufaika na huduma za kiafya za bure chini ya mwavuli wa madaktari kutoka hopspitali ya Mater na ile ya rufaa ya Kenyatta.
Mpango huo uliiongozwa na Elijah Mwangi Foundation uliwalenga walio na dosari za kimwili za aina tofauti tofauti.
Kulingana na Elijah aliyeongea wakati wa hafla hiyo ameichangamoto serikali ya jimbo la Nakuru kuwapelekea wananchi huduma za kiafya karibu akitaja visa vya baadhi ya waathiriwa wa aina mbalimbali ambao hawajapokea huduma za afya licha ya kitengo hicho cha afya kugatuliwa.
"Tumeweza kuwahudumia watu mia tatu na siwezi kukoma kwa sababu madaktari wangu wako tayari kutoa huduma kwa wakaazi ambao hawawezi kujikimu kulipia matibabu," alisema Bw Elijah.
Hata hivyo ametaja haja ya kuhakikisha kuwa vituo vya matibabu kote nchini vina dawa za kutosha kuthibiti afya ya idadi kubwa ya wananchi inayoongezeka kila kuchao.