Wakaazi wa kijiji cha Ngenia, eneo bunge la Kuresoi kaskazini wanalalamika kufuatia ongezeko la visa vya wizi wa mifugo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na wakazi hao wizi wa mifugo sasa umekua jambo la kawaida katika eneo hilo jambo ambalo linawagadhabisha.

"Wiki moja haipiti kabla mifugo haijaibiwa kwenye kijiji hiki, juhudi za kukabiliana na wezi hawa zinagonga mwamba maana wanakuja kama wamejihami kwa silaha," alisema Zachariah Nd'ungu.

Wenyeji wanalaumu uzembe wa vyombo vya usalama.

"Hakuna hatua ambayo polisi wanaonekana kuchukua hata baada ya kuripoti visa vingi, hatujui tutaelekea wapi sasa," Martha wanjiku aliongeza.

 Wakazi hao sasa wametishia kuchukua hatua mikononi mwao iwapo serikali haitaskiza kilio chao.