Shirika la kusambaza nguvu za umeme (Kenya Power) sasa limewataka wananchi wanaoishi karibu na nyaya zinazosambaza umeme kwa kiwango cha juu kuhama kutoka maeneo hayo haraka iwezekanavyo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa anayesimamia maswala ya dharura katika kampuni hiyo tawi la Industrial Area viungani mwa mji wa Nakuru Leonard Matere kwenye mahojiano na mwandishi huyu Jumatano afisini mwake alitoa tahadhari hiyo akisema wakaazi hao wanahatarisha maisha yao hasua wakati huu wa mvua kubwa na mafuriko.

‘ Mawaidha yangu kwa wakenya wanaoishi karibu na nyaya za nguvu za umeme na hasua zinazosambaza umeme wa kiwango cha juu kuhama haraka iwezekanavyo.

Amesema kuwa tayari makaazi hayo yaliyo karibu na nyaya hizo za yamewekwa alama ya kuonyesha kuwa yanafaa kubomolewa.

‘Makaazi hayo yamewekwa alama ya kuonyesha yanafaa kubomolewa. Ukifika katika maeneo ya Kwa Rhonda na Ponda Mali, utaona makaazi hayo yakiwa na alama hiyo. Kenya Power pia imewaambia wakaazi hao sio salama kwao kuishi hapo, aliongeza Matere

Matere alisisitiza kuwa licha ya wakaazi hao kutakiwa kuchukua hatua hiyo mara kwa mara, wamekuwa wakikaidi agizo hilo.

Alisema ingawa kampuni hiyo imeweka mikakati kadhaa ya kukabiliana na hali ya dharura, ni wananchi wanaofaa kuchukua hatua za mapema ili kuzuia majanga yanayoweza kutokea.

Mmoja wa wananchi wanaoishi karibu na nyaya zinazosambaza umeme kwa kiwango cha juu mjini Nakuru, Elijah Wachira, alikiri kupokea onyo hilo kutoka kwa kampuni ya Kenya Power na ile ya kusambaza mafuta ya Kenya Pipeline.

Hata hivyo , analalama kuwa licha ya kutakiwa kuchukua hatua hiyo, kampuni husika zimekosa kuweka mikakati ya kuwatafutia mahala mbadala pa kuishi.

‘Sina nahali pengine ambapo ninaweza kwenda. Nilianza kufanyia kazi yangu hapa . Mtu akikwambia anataka kubomoa nyumba yako saa hizi, anataka uende wapi? aliuliza Wachira.