Serikali ya kaunti ya Mombasa imewataka wakazi wanaoishi kwenye sehemu zinazoweza kukumbwa na mmomonyoko wa udogo kuhamia sehemu salama wakati huu ambapo mvua kubwa zinaendelea kushuhudiwa kote nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na katibu wa kaunti ya Mombasa Francis Thoya, serikali tayari imejitolea kuwasaidia wakazi watakaothirika kutokana na mvua hizo, akisema kuwa kwa sasa kaunti ya Mombasa imetenga jumla ya milioni ishirini ili kuwasaidia wale watakaokumbwa na athari za mvua hiyo.

Akizungumza Ijumaa kwenye afisi yake, Thoya amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mkazi katika maeneo hatari kuanza kuhamia sehemu salama bila kupoteza mda kwani kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya hali ya hewa eneo la Pwani huenda likakumbwa na mvua kubwa inayoweza kiusababisha mafuriko.

Anasema tayari serikali kupitia imeweka mikakati ya namna watakavyotoa misaada kwa familia zitakazoathrika kutokana na mvua hiyo, akiongeza kuwa kumewekwa njia mbadala za kuweza kushuhulikia mahitaji ya dharura kwa watakaoathirika.

Kaunti ya Mombasa ni mojawapo ya maeneo hapa Pwani ambayo yana ardhi iliyotambarare hivyo basi mvua kubwa zinaponyesha huishia kuingia kwenye sehemu za makazi na kuwahangaisha wenyeji kwani sehemu nyingi hukosa njia za kutoa maji kwenye sehemu hizo.