Spika wa Kaunti ya Kisii Kerosi Ondieki amewaomba wakaazi wa kaunti hiyo kuhudhuria mikutano ya kuchangia miswada.
Akiongea hiyo jana katika hafla ya uziduzi wa bendera ya kaunti Ondieki aliwaomba wakaazi hao kuhudhuria mikutano hiyo ili kutoa mchango wao .
“Katiba ya Kenya imewapa wananchi nafasi ya kuchangia katika miswaada ya kaunti. Wananchi wanastahili kutoa maoni yao kabla ya miswaada kupitishwa katika bunge la kaunti,” alisema Ondieki.
Kulingana na Ondieki wakaazi wengi wa kaunti ya Kisii hususia mikutano hiyo na baada ya sheria hizo kupitishwa wanajitokeza na kusema sheria hizo zina waathiri.
Aidha aliwaomba wakaazi wa Kisii kuungana ili kuinua viwango vya uchumi.
Kerosi aliwapongeza waakilishi wa wadi zote za kaunti kwa kuwa na ushirikiano mwema hasa wakati waliokuwa wakipitisha mswada wa kuwa na bendera ya kaunti.